Kidhargari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidhargari ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wadhargari katika jimbo la Australia ya Magharibi. Mwaka wa 2007, kulikuwa na msemaji wa Kidhargari mmoja tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidhargari kiko katika kundi la Kipama cha Kusini-Magharibi.