Kidhangu-Djangu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidhangu-Djangu ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wadhangu katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kidhangu-Djangu 270. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidhangu-Djangu kiko katika kundi la Kiyolngu.