Kidhalandji
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidhalandji ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wadhalandji katika jimbo la Australia ya Magharibi. Mwaka wa 2008, kulikuwa na wasemaji wa Kidhalandji sita tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidhalandji kiko katika kundi la Kikanyara.