Kidarkinyung
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidarkinyung (au Kidarkinjung) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wadarkinyung katika jimbo la New South Wales. Mwaka wa 2008, kulikuwa na wasemaji wa Kidarkinyung wachache tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidarkinyung kiko katika kundi la Kiyuin.