Kidalabon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidalabon (pia Kingalkbun) ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wadalabon katika ya jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kidalabon kumi na mmoja tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidalabon kiko katika kundi lake lenyewe la Kingalkbun.