Kiyue
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyue (pia Kicantonese) ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina inayozungumzwa na Wayue. Mwaka wa 1984 idadi ya wasemaji wa Kiyue nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu milioni 52. Pia kuna wasemaji katika nchi zifuatazo: 6250 nchini Brunei (2006), 6,030,000 ndani ya Hong Kong (2006), 180,000 nchini Indonesia (1982), 1,070,000 nchini Malaysia (2000), 9780 nchini Ufilipino (2000), 121,000 nchini Singapuri (2010), 29,400 nchini Uthai (1984), na 862,000 nchini Vietnam (1999). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kiyue iko katika kundi la Kichina.