Kibayungu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibayungu ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wabayungu katika jimbo la Australia ya Magharibi. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kibayungu wawili tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibayungu kiko katika kundi la Kikanyara.