Kibarbaram
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibarbaram (au Kimbabaram) ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wabarbaram katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kibarbaram ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibarbaram kiko katika kundi la Kipama cha Kusini.