Kibarababaraba
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibarababaraba ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wabarababaraba katika jimbo la New South Wales. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kibarababaraba watano tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibarababaraba kiko katika kundi la Kikulin cha Magharibi.