Kibadimaya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibadimaya ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wabadimaya katika jimbo la Australia ya Magharibi. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kibadimaya watatu tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibadimaya kiko katika kundi la Kiwadjari, yaani inahusiana na Kiwajarri.