![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/33/Atayal.svg/langsw-640px-Atayal.svg.png&w=640&q=50)
Kiatayal
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiatayal ni lugha ya Kiaustronesia nchini Taiwan inayozungumzwa na Waatayal. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kiatayal imehesabiwa kuwa watu 84,300. Kuna lahaja mbili: Kisquliq na Kic'uli'. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiatayal kiko katika kundi lake lenyewe la Kiatayaliki.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/33/Atayal.svg/220px-Atayal.svg.png)