Kiatampaya
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiatampaya ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waatampaya kwenye rasi ya Cape York katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiatampaya ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiatampaya kiko katika kundi la Kipama cha Kaskazini.