Kiarrernte cha Mashariki
lugha moja ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiarrernte cha Mashariki ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waaranda katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kiarrernte cha Mashariki ilihesabiwa kuwa watu 2380. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiarrernte cha Mashariki kiko katika kundi la Kiarandiki.