Kiareba
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiareba ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waareba katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiareba ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiareba kiko katika kundi la Kipama cha Norman.