Kiarabana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiarabana ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waarabana katika jimbo la South Australia. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kiarabana ilihesabiwa kuwa watu kuminawawili tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiarabana kiko katika kundi la Kipalku.