Kiantakarinya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiantakarinya ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waantakarinya katika jimbo la South Australia. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kiantakarinya ilihesabiwa kuwa watu sita tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiantakarinya kiko katika kundi la Kiwati.