Kianguthimri
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kianguthimri ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waanguthimri kwenye rasi ya Cape York katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kianguthimri ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kianguthimri iko katika kundi la Kipama cha Kaskazini.