Kiandagerebinha
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiandagerebinha ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waandagerebinha mpakani katikati ya majimbo ya Northern Territory na Queensland. Mwaka wa 2005, idadi ya wasemaji wa Kiandagerebinha ilihesabiwa kuwa watu watano tu, yaani lugha iimekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiandagerebinha kiko katika kundi la Kiarandiki.