Kiamurdak
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiamurdak (au Kiamurdag) ni lugha ya asili nchini Australia inayozungumzwa na Waamurdak katika jimbo la Northern Territory. Mwaka wa 2007, kulikuwa na msemaji mmoja wa Kiamurdak tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiamurdak kiko katika kundi la Kiamaragiki. Wengine hukihesabu kama lugha ya Kiiwaidjan.