Kialyawarr
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kialyawarr ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waalyawarr katika jimbo la Queensland. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kialyawarr ilihesabiwa kuwa watu 1660. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kialyawarr kiko katika kundi la Kiarandiki.