Kialngith
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kialngith ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waalngith kwenye rasi ya Cape York katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kialngith ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kialngith iko katika kundi la Kipama cha Kaskazini.