Kiaghu-Tharnggala
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiaghu-Tharnggala (pia Kiaghu-Tharnggalu) ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waaghu-Tharnggala kwenye rasi ya Cape York katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiaghu-Tharnggala ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiaghu-Tharnggala iko katika kundi la Kipama cha Rarmul.