Kiadithinngithigh
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiadithinngithigh (pia Kiadetingiti au Kiaritinngitigh) ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waadithinngithigh kwenye rasi ya Cape York katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiadithinngithigh ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiadithinngithigh iko katika kundi la Kipama cha Kaskazini.