From Wikipedia, the free encyclopedia
Kali (pia: potasiamu, ing. potassium) ni elementi na metali alikali yenye namba atomia 19 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 39.098. Alama yake ni K.
Kali (kalium; potassium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Kali (kalium; potassium) |
Alama | K |
Namba atomia | 19 |
Mfululizo safu | Metali alikali |
Uzani atomia | 39.098 |
Densiti | 0.89 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 336.53 K (63.38 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 1032 K (759 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 2.4 % |
Hali maada | imara |
Jina Kali latokana na neno la Kiarabu "qalia" kwa majivu lakini jina la potasiamu ni kawaida vilevile kutokana na neno "potassium" kwa sababu kampaundi zake zimo kwa wingi ndani ya majivu ya ubao yaliyosafishwa kwa kuchemsha katika sufuria (Kiing.: "ash" na "pot").
Kali (potasiamu) ni metali laini sana inayochemka kwa sentigredi 83 tayari. Rangi yake ni nyeupe-fedha. Haipatikana kiasili kama metali tupu kwa sababu humenyuka haraka na kuoksidika hewani. Inamenyuka vikali sana na maji hivyo kali metali hutunzwa chini ya mafuta.
Aloi ya kali na natiri hutumiwa kama kiowevu cha kupoza mitambo ya nyuklia.
Chumvi za kali hutumiwa sana kama mbolea wa kilimo.
Kali (Potasiamu) ni muhimu hasa katika chembe za mimea na wanyama. Lazima kuwepo katika chakula chetu lakini si mno kwa sababu ikizidi inaleta hasara.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.