![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0c/Jupiter_Tonans.jpg/640px-Jupiter_Tonans.jpg&w=640&q=50)
Jupiter
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jupiter (pia: Iuppiter, Iovis) ni mkuu wa miungu katika dini ya Roma ya Kale. Analingana na Zeu katika dini ya Ugiriki ya Kale.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0c/Jupiter_Tonans.jpg/640px-Jupiter_Tonans.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d6/Blitzbuendel_02.jpg/640px-Blitzbuendel_02.jpg)
Kiasili Jupiter aliabudiwa kama mungu wa hali ya hewa aliyetawala radi na ngurumo. Baadaye alipewa nafasi ya baba wa miungu na pia wa wanadamu. Nembo yake ni radi anayoishika mkononi kwa sababu aliaminiwa ni mwenye uwezo wa kuzirusha.
Jupiter alikuwa na hekalu kubwa kabisa kwenye kilima cha Kapitoli mjini Roma penye mahekalu muhimu.
Katika utamaduni wa Kiroma sayari Mshtarii ilitazamiwa kama alama ya mungu huyu angani na sayari aliitwa kwa jina la Jupiter. Lugha nyingi za Kiulaya zinaendelea kutumia jina kwa sayari hii.