Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Joseph Smith, Mdogo (23 Desemba 1805 - 27 Juni 1844) alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa Wamormoni.
Mwaka wa 1827 alidai kuwa malaika alimtokea na kufunulia maagizo ya Mungu katika kitabu kipya, yaani Kitabu cha Mormoni. Mwaka wa 1830 alikichapisha kitabu hicho.
Miaka ya 1830, makao makuu ya Wamormoni yalianza jimboni Ohio, baadaye jimboni Missouri na kuanzia mwaka wa 1838 jimboni Illinois. Pale Smith Mdogo alitawala kama mwenyekiti wa kijiji mpaka alipouawa na umati wa watu wasiokubali utawala wake.
Alifuatwa kama kiongozi wa Wamormoni na Brigham Young aliyewaongoza Wamormoni kuhamia jimbo la Utah.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.