Illizi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Illizi (Kiarabu:إليزي) (wakazi. 10,163) ni mji uliopo kusini-mashariki mwa sehemu ya nchi ya Algeria. Huu ni mji mkuu wa Jimbo la Illizi. Ni moja kati ya milango ya kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Tassili N'Ajjer kwenye mapango ya mchanga yaliyo na michoro ya kale na tarehe kuanzia miaka 6 000 KK. Kuna hoteli na sehemu mbili ya kuwa kambi za watalii, na vilevile mawakala kibao wa watalii.