Ibrahima Konaté
Mchezaji mpira wa miguu wa Ufaransa / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ibrahima Konaté (alizaliwa Paris[1], 25 Mei 1999[2]) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutokea nchini Ufaransa ambaye anacheza kama beki wa kati katika klabu ya Liverpool F.C. inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza (EPL) na timu ya taifa ya Ufaransa. Akianzia na klabu Sochaux, Konaté alihamia RB Leipzig mwaka 2017. Baada ya miaka minne na klabu hiyo, Liverpool ilimsajili mwaka 2021 kwa ada ya paundi milioni 36. Alishinda kombe la EFL na kombe la FA katika msimu wake wa kwanza.