![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2c/Egypt.Edfu.Temple.01.jpg/640px-Egypt.Edfu.Temple.01.jpg&w=640&q=50)
Horus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Horus alikuwa mmoja wa miungu ya Misri ya Kale. Katika mitholojia ya Kimisri alikuwa mwana wa Isis na Osiris. Aliabudiwa hasa kama mungu wa anga na pia mungu wa ufalme.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2c/Egypt.Edfu.Temple.01.jpg/640px-Egypt.Edfu.Temple.01.jpg)
Ibada yake iliendelea kwa muda mrefu, kuanzia nasaba ya kwanza hadi wakati wa Misri ya Kiroma. Katika kipindi hicho mawazo mengi kuhusu Horus yalitokea akaabudiwa kwa maumbo mengi tofauti.
Lakini umbo kuu lilikuwa ndege ya kozi au mwanadamu mwenye kichwa cha kozi.
Horus, aliabudiwa kote Misri, haswa huko Pe, Bendet na Khem .