Quintus Horatius Flaccus (pia: Horasi; 8 Desemba 65 KK - 27 Novemba 8 KK) alikuwa mshairi mashuhuri wa Roma ya Kale.

Thumb
Sanamu ya Horasi mjini Verona, Italia.

Alizaliwa kama mtoto wa mtumwa aliyepewa uhuru na bwana wake na kutajirika baadaye. Hivyo aliweza kumpa mwanawe elimu nzuri. Alisomea Roma na baadaye Ugiriki.

Aliandika mengi kwa lugha ya Kilatini akasifiwa wakati wake na katika karne zilizofuata.

Kati ya maneno yake yaliyorudiwa mara kwa mara ni:

  • Sapere aude! - "Thubutu kujua" (yaani: Ujiamini kutumia akili!)
  • Dulce et decorum est pro patria mori - "Ni tamu, tena inafaa, kufa kwa nchi yako."
  • Carpe diem - "Shika siku" (yaani: Usipoteze fursa za kufurahia leo!)

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.