HTML
From Wikipedia, the free encyclopedia
HTML ni kifupi cha "HyperText Markup Language" au Lugha ya kutunga matini ya mtandao. Ni aina ya lugha ya matinikivo (hypertext) inayotumiwa ili wavuti uonekane mtandaoni jinsi inavyotakiwa. HTML ni lugha ya matinikivo inayotumiwa zaidi kwenye wavuti wa walimwengu (WWW).
Ni mchanganyiko wa lugha ya kawaida na misimbo ya pekee inayoieleza tarakilishi kuonyesha maandishi, picha au rangi kwa namna fulani jinsi inavyotakiwa.
Programu ya kivinjari (au kisakuzi - "browser") kama Firefox au Internet Explorer inasoma lugha hii ya HTML inapoambiwa jinsi gani kuonyesha ukurasa. Ukurasa wa wavuti unaweza kuonyesha maandishi, viungo, picha au hata sauti na video.