Go-Nijo wa Japani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Go-Nijo (9 Machi, 1285 – 10 Septemba, 1308) alikuwa mfalme mkuu wa 94 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Kuniharu, na alikuwa mwana wa kwanza wa Go-Uda. Mwaka wa 1301 alimfuata binamu yake Go-Fushimi, na kuwa mfalme hadi kifo chake 1308. Aliyemfuata kama Tenno ni binamu yake Hanazono.