Fanani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fanani ni mtu ambaye anawasilisha kazi za fasihi kwa hadhira.
Kwa mfano, mwimbaji anawaimbia watu ukumbini, hivyo fanani ni mwimbaji kwani anawasilisha ujumbe aliokuwanao kwa jamii, na hadhira ni watu wanaomsikiliza mwanamuziki kwani hawa hupokea ujumbe kuhusu jambo fulani kutoka kwa fanani.
Mifano mingine ya fanani, pamoja na mwimbaji, ni mwigizaji, mtangazaji, msimuliaji n.k.