Digidigi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Digidigi | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Digidigi wa Kirk (Madoqua kirkii) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 4, nususpishi 9:
| ||||||||||||||||
Funga
Digidigi ni wanyamapori wadogo wa jenasi Madoqua katika familia Bovidae. Wanyama hawa ni miongoni mwa wanyama wadogo kabisa wa Bovidae (kimo sm 30–40 begani, urefu sm 50–70 na uzito kg 3–6). Wanatokea savana kavu za Afrika kusini kwa Sahara. Jike ni mkubwa kidogo kuliko dume lakini dume ana pembe fupi na nyembamba. Wana ushungi kwa utosi unaoficha pengine pembe za dume. Rangi yao ni ya mchanga lakini mgongo una rangi ya majivu. Digidigi hula majani, matunda na beri. Wanapata maji ya kutosha kutoka chakula chao, kwa hivyo hawana haja ya kunywa.