From Wikipedia, the free encyclopedia
Mpingo (Dalbergia melanoxylon) ni mti mdogo wenye ubao ulio mweusi kwa ndani ambao hutumika kutengeneza samani, sanamu na vipande vya ala za muziki kama nzumari, filimbi za Wazungu na mirija ya bagpipes. Ubao pia huitwa mpingo. Mara nyingi huitwa abunusi, lakini jina hili si sahihi; hii ni ubao wa mgiriti au mgombe (Diospyros mespiliformis).
Mpingo (Dalbergia melanoxylon) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Ubao huo ni mzito na mgumu sana upande wa ndani na huo ubao mweusi umetafutwa tangu siku za kale. Ubao wa nje una rangi kahawia-njano ni nyepesi na laini hauna thamani sana.
Mpingo una ushahidi katika Biblia kama bidhaa iliyopelekwa kutoka mbali, katika kitabu cha Ezekieli mlango wa 27,5 "mpingo" (הָבְנִים - håvnîm) unatajwa kama bidhaa iliyochukuliwa kutoka mji wa Dedani katika Uarabuni; ilhali mti haujulikani Uarabuni bali ni mti wa Afrika pekee inaonekana ilichukuliwa na Wadedani kutoka upande mwingine wa Bahari ya Shamu.
Mpingo wa Dalbergia melanoxylon ni mti wa Afrika ambao ni tofauti na mpingo wa Kihindi wa jenasi Diospyros. Zamani aina hizi mbili zilichanganywa na hii inaonekana kutokana na jina "ebony" katika lugha ya Kiingereza kwa mpingo wa Kihindi ingawa neno hili linatokana na Kimisri cha kale hbny na Kigiriki ἔβενος (ebenos). Neno hili la Wamisri wa Kale lilitaja ubao wa mpingo wa Dalbergia melanoxylon jinsi unavyopatikana katika makaburi ya Misri ya Kale.[1]
Ubao wa mpingo hutafutwa sana hadi leo kwa hiyo miti inakatwa mno ni mti unaohatarishwa. Katika Tanganyika wakoloni Wajerumani walianza kuvuna mpingo kwa kiasi kikubwa na Waingereza waliendelea kuvuna miti mingi. Tangu miaka ya 1980 mti ulionekana uko hatarini ya kupotea na serikali ya Tanzania ilikataa kuuuza nje. Hata hivyo mahitaji ya wachongaji wa ubao kwa ajili soko la utalii yaliendelea kusababisha kukatwa kwa miti mingi na siku hizi miti mikubwa imekuwa haba sana. Kama mavuno ya ubao unaweza kubanwa zaidi wataalamu wanaona nafasi nzuri ya kupoa kwa mpingo.[2]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.