Cluny
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Abasia ya Cluny (au Cluni, au Clugny), ilikuwa monasteri ya Wabenedikto, maarufu kwa kuongoza urekebisho wa utawa na wa Kanisa lote kuanzia karne ya 10.
Ilijengwa kwa mtindo wa Kiroma katika eneo la Burgundy, leo mkoa wa Saône-et-Loire, Ufaransa.
Mwanzilishi wake, William I wa Aquitania, mwaka 910 alimteua Berno wa Cluny awe abati wa kwanza, chini ya Papa Sergius III tu. Hivyo alionyesha njia ya kukwepa watawala wasiendelee kuingilia vyeo vya Kanisa kwa malengo yao ya kisiasa na ya kiuchumi badala ya yale yaliyokusudiwa ya kidini.
Monasteri nyingine nyingi zilifuata njia hiyo na kivyo kuinua hali ya kiroho ya utawa na wa Kanisa kwa jumla katika karne zilizofuata.
Mwaka 1790, wakati wa Mapinduzi ya Kifaransa, abasia iliporwa na kubomolewa kwa kiasi kikubwa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.