From Wikipedia, the free encyclopedia
Chokoleti ni pipi au chakula kitamu kinachotengezwa kwa kutumia kakao, sukari na mafuta. Jina hilo linatumiwa pia kwa kinywaji cha kakao.
Asili yake ni kinywaji cha watu wa Mexiko wa kale waliochemsha unga wa kakao katika maji pamoja na viungo. Wahispania waliikuta kwa Azteki na kuipeleka Ulaya, wakitumia jina la Kiazteki "xocolātl" lenya maana ya "maji machungu".
Katika Ulaya ilitumiwa muda mrefu kama kinywaji, na wakati wa karne ya 19 Wajerumani walianza kutengeneza pipi jinsi inavyojulikana leo.
Chokoleti huyeyuka haraka kwa sentigredi 40-50, hivyo ni rahisi kuifinga kwa maumbo mbalimbali.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chokoleti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.