Chengdu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Chengdu ni jiji kubwa la nne nchini China ikiwa na wakazi wapatao milioni 14 hadi 15.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/9/9c/Chengdu_montage.png)
Ni makao makuu ya jimbo la Sichuan na kitovu muhimu cha uchumi na utamaduni magharibi mwa China.
Chakula chake ni mashuhuri na watu wake hupenda pilipili. Kimataifa ni mashuhuri ikiwa kituo cha utafiti wa panda mkubwa.