Bié (mkoa)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bié ni mkoa wa Angola wenye eneo la km² 70,314 na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya lakhi nane na milioni moja.
![Mkoa wa Bie katika Angola](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/f/f8/Angola_Provinces_Bie_250px.png)
Makao makuu ya mkoa yako mjini Kuito (Cuito).
Hali ya hewa haina joto kali kutokana na milima na mvua ya mara kwa mara. Hayo yote huwezesha kilimo cha mahindi, karanga, miwa, kahawa na mpunga.
Mkoa ni sehemu ya Nyanda za Juu za Bie. Kuna njia ya reli kati ya mkoa na pwani.
Miji mikubwa zaidi mkoani ni:
- Kuito- wakazi 114 791
- Camacupa- wakazi 19 347
- Catabola- wakazi 19 281
- Catumbela- wakazi 17 369
- Chisamba- wakazi 7 755
Nyumba ya mwenyekiti wa chama cha UNITA Isaias Samakuva iko mkoani kwenye mji wa Kunji.