Berd
From Wikipedia, the free encyclopedia
Berd (kwa Kiarmenia: Բերդ; zamani uliitwa: Berrdagyugh, Berrdgyugh, T’avuzghala, T’auzk’end, T’ovuz, T’ous, Taua Kale, T’auzkala, Taya-Kala, Tovuzkala, Bert, T’ous Gale, Volorut, Shlorut, Ghalak’yand, na T’uzukala) ni mji uliopo nchini Armenia kwenye mkoa wa Tavush. Mji huu huhesabiwa kama kitovu cha kanda ya maeneo ya Shamshadin. Upo upande wa kushoto mwa mto Tavush, takribani kilomita 211 kutoka mjini Yerevan. Mji umezungukwa na vilima.