From Wikipedia, the free encyclopedia
Ardahan (Kirmenia: Արդահան; Kirusi: Ардаган; Kigeorgia: არტაანი) ni mji uliopo mjini kaskizini-mashariki ya nchi ya Uturuki, ambao umepakana na mpaka wa nchi ya Georgia. Huu ni mji mkuu wa Mkoa wa Ardahan.
Ardahan ni mji mkuu mdogo kuliko yote katika Uturuki, hadi kufikia 1993, ulikuwa mji mdogo wa mkoa jirani wa Kars. Tangu kugawiwa kwa kata za mkoa kumekuwa na uwekezaji mwingi na kumekuwa na majengo mengi ya serikali, lakini maisha ya huko na ya kuishi juu ya milima na kuna kuwa na saluji kwa muda wa nusu mwaka lakini bado watu wangaliishi huko. Kuna mahoteli mengi tu, ambayo mara nyingi hutumika kwa madereva wa magari makubwa na wale wsafiri waelekeao Georgia.
Chuo Kikuu cha Kars Kafkas kina taasisi katika mji wa Ardahan na kuna makazi pia ya wanajeshi. Raia wa kawaida, wanafunzi na wanajeshi wameweka kambi yao hapo ili kusaidia hali ya uchumi ya mji huo. Watu hao wana vilabu vyao na majumba ya wageni, wakati huko mjini kwenyewe kuna mambo machache yahitajikanayo kwa jamii, zaidizaidi kuna vijiduka kadhaa vya kuuza keki na mgahawa chai na kababu. Kwenda kununua bidhaa kubwakubwa nazo hamna.
Sherehe Muhimu za Huko
Siku Kuu
Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ardahan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.