From Wikipedia, the free encyclopedia
Panzi ni aina za wadudu wanaokula mimea. Wameainishwa katika nusuoda Caelifera ya oda Orthoptera. Takriban spishi zote huchupa mbali kwa kutumia miguu yao ya nyuma ambayo ina nguvu sana. Nyingi zinaweza kuruka angani. Panzi wana vipapasio vifupi kuliko mwili wao. Panzi wakubwa ambao wanajikusanya kwenye makundi makubwa huitwa nzige. Kuna panzi wakubwa wengine wenye miiba mikubwa kwenye miguu ya nyuma lakini wasiojikusanya katika makundi. Panzi hao hufanana na ndege wadogo wakiruka juu na huitwa parare.
Panzi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Panzi kibyongo, Abisares viridipennis | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Oda za chini 2:
| ||||||||||||||
Panzi majike wana vali mwichoni kwa fumbatio zinazowawezesha kuchimba ndani ya ardhi na kutaga mayai yao katika vibumba. Vibumba vya mayai huweza kuwa na mayai kumi na tano hadi zaidi ya mia moja. Mayai ya spishi nyingi za panzi huingia kwa diaposi kupitia majira ya baridi au kiangazi. Hali ya hewa ikiwa nzuri mayai yaendelea kupevuka halafu tunutu wanatoka. Tunutu (panzi wachanga bila mabawa) hubambua ngozi yao mara tano hadi mara saba kufuatana na spishi. Kila hatua ya ukuaji ni ndefu kuliko ile iliyotangulia. Wakati wa ubambuaji wa mwisho panzi wenye mabawa anatoka na kuwa mpevu ndani ya siku au wiki chache.
Kuna wadudu ambao wanafanana na panzi lakini wana vipapasio virefu kuliko mwili wao. Hawa ni wana wa nusuoda Ensifera. Spishi moja kati yao anaitwa senene na huliwa na watu. Jike ana mrija wa kutaga unaofanana na kitara. Anataga mayai juu ya au ndani ya mimea.
Panzi huliwa sehemu nyingi duniani kwa sababu wana virutubishi vya (protini) vingi. Wanajeshi huambiwa wakamate panzi na kuwala wakipungukiwa chakula.
Kuna familia nyingi za panzi, lakini takriban spishi zote za Afrika ya Mashariki ni wanafamilia wa Acrididae na Pyrgomorphidae. Mwainisho wa sikuhizi ni kama ufuatao (familia zote hazionyeshwi):
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.