Abd el Kader
From Wikipedia, the free encyclopedia
Abd el Kader (6 Septemba 1808 – 26 Mei 1883), (Kiarabu عبد القادر ابن محيي الدين ʿAbd al-Qādir ibn Muḥyiddīn; alijulikana pia kama Abdul Qadir, Emir Abdelkader au Abdelkader El Djezairi), alikuwa kiongozi wa kijeshi, wa kidini na wa kisiasa nchini Algeria.
Alipigana dhidi ya uvamizi wa Ufaransa katika Algeria kuanzia mwaka 1830 hadi 1847. Baada ya kushindwa aliishi Dameski na hapo aliingilia katika ghasia ya mwaka 1860 alipookoa Wakristo wengi waliotishiwa na mauaji.