Mwalimu wa Kanisa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mwalimu wa Kanisa

Mwalimu wa Kanisa ni jina la heshima ambalo kwa nadra Kanisa Katoliki linampa mtakatifu ambaye katika maisha, mafundisho na maandishi yake alionyesha na kueneza mwanga wa pekee katika masuala ya imani, maadili na maisha ya kiroho.

Walimu wa Kanisa wa kwanza kutangazwa walivyochorwa na Pier Francesco Sacchi mwaka 1516 hivi. Kwa sasa mchoro unatunzwa huko Paris, Ufaransa. Kuanzia kushoto mbele: Agostino wa Hippo, Papa Gregori I, Jeromu na Ambrosi wa Milano.

“Tamko la kwamba mtakatifu fulani ni Mwalimu wa Kanisa lote linategemea utambuzi wa karama maalumu ya hekima ambayo alijaliwa na Roho Mtakatifu kwa faida ya Kanisa ikabainishwa na athari njema ya mafundisho yake katika Taifa la Mungu” (Papa Benedikto XVI, Barua ya Kitume ya tarehe 7 Oktoba 2012).

Utaratibu

Jina hilo linatolewa na Papa au Mtaguso. Mpaka sasa, katika miaka karibu 2000 ya historia ya Kanisa wanaume 32 na wanawake 4 tu wamepewa heshima hiyo.

Wa kwanza kutangazwa (mwaka 1298) ni mababu wa Kanisa wanne muhimu zaidi upande wa Magharibi: Ambrosi wa Milano, Agostino wa Hippo, Jeromu na papa Gregori I.

Mwaka 1568 walitangazwa mababu wa Kanisa wanne muhimu zaidi upande wa Ukristo wa Mashariki: Atanasi wa Aleksandria, Basili Mkuu, Gregori wa Nazienzi na Yohane Krisostomo, pamoja na Thoma wa Akwino, mwalimu bora wa Karne za Kati upande wa Ukristo wa Magharibi.

Halafu mapapa wakaendelea kuongeza wengine. Wa mwisho kutangazwa kwa sasa ni Gregori wa Narek (12 Aprili 2015).

Orodha

Mwaka wa kutangazwa ukifuatwa na nyota unaonyesha watakatifu wanaoheshimiwa na Waorthodoksi pia, ingawa kwao hakuna cheo cha mwalimu wa Kanisa.

Marejeo kwa Kiswahili

  • Masomo ya Breviari - ed. Ndanda Mission Press - Ndanda 1978
  • Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1989
  • MAURICE SOSELEJE – Kalendari Yetu Maisha ya Watakatifu – Toleo la Pili – ed. Benedictine Publications Ndanda-Peramiho – Ndanda 1986 - ISBN 9976-63-112-X
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.