Dagaa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Dagaa ni jina la kawaida la samaki wa oda Clupeiformes isipokuwa spishi za familia Chirocentridae. Spishi nyingi zina majina mengine pia, kama vile kapenta, kerenge, lumbu, mbarata, mwatiko, ndakala, pata, pawali, simu, uono na usipa. Spishi kadhaa za familia Alestidae, Apogonidae, Atherinidae, Cyprinidae na Leiognathidae huitwa dagaa pia lakini majina mengine yanapendelewa. Dagaa wanatokea katika bahari zote za dunia na katika maziwa na mito mingi.
Dagaa | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dagaa-papa tumbo-laini (Amblygaster leiogaster) | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Familia 5:
| ||||||||||
Kibofuhewa cha Clupeiformes kimeungana na utumbo kwa kifereji. Kwa kawaida hawana mrabafahamu (mstari wa ubavu, lateral line kwa Kiingereza) lakini wana macho, mapezi na magamba ambayo ni ya kawaida kwa samaki wengi, ingawa siyo samaki wote wana sifa hizi. Wao ni samaki wenye rangi ya fedha na mwili mwembamba wenye umbo la dulabu, na mara nyingi huunda makundi. Takriban spishi zote hula planktoni ambazo huzichuja kutoka kwa maji kwa matamvua yao.